Friday, February 25, 2011

CHADEM JIJINI MWANZA








CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kililiteka Jiji la Mwanza, pale viongozi wake wa kitaifa walipoongoza maelfu ya waandamanaji katika Jiji hilo.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa na wabunge kadhaa waliowaongoza maelefu ya wandamanaji katika kile walichosema kuwa ni kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.

Katika mkututano wa hadhara uliohitimishwa katika Viwanja vya Furahisha, Dk Slaa alitoa siku tisa kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuhusu kushamiri kwa vietndo vya ufisadi, malipo ya Dowans na suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha kwa Watanzania.

Dk Slaa alisema iwapo Serikali itakaa kimya basi Chadema kitaitisha maandamano ya nchi nzima ili kushinikiza mabadiko kama ilivyo katika nchi za Misri na Tunisia.

Alisema kitendo cha Rais Kikwete kuendelea kukaa kimya kitasababisha Chadema kuchukua hatua ya pili ambayo wataitisha maandamano nchi nzima.

Kabla ya mkutano huo, kulikuwa na maandamano yaliyoanzia katika Uwanja wa Shule ya Msingi Buzuruga na kupita katika Barabara za Nyerere, Pamba na kuingia Barabara ya Kenyatta na ile ya Uwanja wa Ndege na kuhitimishwa katika Uwanja wa Furahisha.

Wakipita katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza, waandamanaji walikuwa na mabango wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa kuilaumu Serikali kutokana na kile walichosema kuwa ni kufumbia macho ufisadi.

Aidha, akizungumzia suala la Dowans, Dk Slaa alisema kamwe kodi ya wananchi haitotumika kuilipa kampuni hiyo na kwamba kama wanataka kampuni hiyo kulipwa basi zitumike fedha za Rais Kikwete,Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

Alisema ujio wa mmiliki wa Dowans, Suleyiman Al Adawi ni mbinu za kutaka kuwahadaa Watanzania.

“Dowans haiwezi kulipwa kwa kodi za wananchi kutokana na kampuni hiyo kuwa mtoto haramu, mama na baba yake ni Richmond na hayo yote yanayofanyika Rais Kikwete anayajua sababu yanafanyikia katika Serikali ya Tanzania, ”alisema Dk Slaa.

Alisema Rais Kikwete ana maswali mengi ya kujibu kutokana na Dowans kwa sababu Serikali ilitoa fedha nyingi za wananchi za kuleta mitambo hiyo ya umeme na kununua vifaa ili Dowans izalishe umeme, lakini leo nchi ipo gizani.

Kupanda kwa gharama za maisha
Katika hatua nyingine, Dk Slaa alisema kupanda kwa gharama za maisha kunatokana na kupanda kwa umeme pia kukatika kwa umeme ambapo uzalishaji haufanyiki kama inavyotakiwa.

Alisema tabia ya wabunge wa CCM kuwazomea na kuwatisha wabunge wa Chadema wasiongee bungeni ni kazi bure na kusema kuwa kama hawatojirekebisha kwa hilo watawahamasisha wananchi kuwazomeoa wabunge hao majimboni kwao kama ilivyokuwa kipindi kile cha EPA.

Dk Slaa pia alimtahadharisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro kutokuingilia mamlaka ya Halmashauri ya Jiji na badala yake amuachie Meya wa Jiji hilo ambaye ni kutoka Chadema afanye kazi kwani yeye ndiye aliye na mamlaka hayo.

Alisema kwa mujibu wa sheria namba 19 ya mwaka 1999 inamtaka Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya kuwa wawezeshaji na sio watu wa kuingilia mamlaka ya Halmashauri ya Jiji.

Mbowe aonya Serikali kuhusu ufisadi
Kwa upande wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kama Serikali haitaweze kuinua maisha ya Watanzania kwa kuwaondolea ugumu wa maisha, wananchi wanaweza kutumia nguvu kukabiliana na mafisadi.

Wakatia akihutubia adhara hiyo ya watu waliokusanyika katika mkutano huo, Mbowe aliwaomba wananchi hao kuelezea Serikali kuwa wapo tayari kudai haki zao na kusema kuwa viongozi wa Chadema wakiongea CCM wanasema kuwa wanawaongopea wananchi kuwa hawajawatuma.

“Tumenyanyaswa, tumetishwa sasa tunasema kuwa tumechoshwa na tunasonga mbele kudai haki pamoja na uhuru na kama hawatoweza kutupatia nguvu zetu zitakuwa zaidi ya Libya," alisema Mbowe.

“Mnataka na Kikwete ajiuzulu pia,” wananchi walimjibu kwa sauti “Ndiyo” Mbowe aliendela na kusema, “Sawa nimewaelewa kumbe mnataka Rais Kikwete naye ajiuzulu pamoja na Ngeleja na Waziri Mwinyi (Hussein) pia ajiuzulu..ahaa ngojeni kwanza Kikwete tunataka kwanza tumalize kupita mahali pote na kuzunguka yeye inakuja yake babu kubwa kama ya Misri na Tunisia,” alieleza Mbowe.

Alisema Serikali ipo katika mpango wa kukodisha umeme kwa muda wa miezi minne na katika kipindi hicho wanazalisha umeme kwa kutumia kodi za Watanzania Sh 400 bilioni kulipa kampuni inayokodisha mitambo hiyo ya umeme.

Alisema Serikali kukubali kulipa Sh 300 bilioni za kunulia mafuta ni wizi mkubwa na kwamba uvumilivu wa Watanzania umefikia ukomo hivi sasa.

"Tumevumilia vya kutosha, safari hii ni ama zao ama zetu. Hatuwezi kukubali nchi imekaa miaka minne hakuna ufumbuzi wa umeme, taifa linalipa fedha za ajabu, hakuna anayejiuzulu na safari hii hatukubali,"alisema Mbowe na kuongeza:

"Mkuu wa Mkoa anatumia jenereta, Waziri Ngeleja, Waziri Mkuu wote hawa hawajui shida ya umeme, shida iko kwetu wananchi hivyo wananchi lazima tuchukue hatua".

Baada ya hapo aliwauliza wananchi iwapo wanataka Waziri Ngeleja ajiuzulu, wananchi walijibu ajiuzulu na kumtaja Rais Kikwete pia kujiuzulu.

Katiba ya nchi

Mbowe alisema aliwaongoza wabunge kutoka nje kumfikishia Rais Kikwete kutaka mabadiliko na kwamba hatua ile ilibezwa na viongozi wa CCM ambao leo hii wanaushangaza umma kwa kujadili mabadiliko ya Katiba.

Alisema baada ya hatua hiyo, mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika aliwasilisha bungeni hoja kuhusu suala hilo, lakini haikuweza kujadiliwa na hivyo kuwataka wananchi kuvumilia kwa vile sasa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya utaanzia bungeni Aprili mwaka huu.

Joseph Mbilinyi na Halma Mdee
Kwa upande wake, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema kuwa Tanzania haina amani kama Serikali ya CCM inavyowatangazia wananchi.Alisema anashangaa hata wabunge wakiingia bungeni wanakaguliwa, sasa je wananchi wa mitaani.


Jonh Mnyika na Godbless Lema
Pamoja na kuambiwa kumuobaa radhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisisitiza kauli yake kuwa alidanganya na kusema kuwa kamwe hawezi kuomba radhi.

Alisema Jeshi la Polisi mkoani Arusha liliomba siku 60 kufanya upelelezi wa mauaji yaliyotokea jimboni kwake, inakuwaje leo anasimama na kuwadanganya wananchi kuwa Chadema ndiyo waliofanya mauaji hayo wakati hata upelelezi haujakamilika.

Kwa upande wake, Mnyika alisema kupanda kwa gharama za maisha ni matokeo ya mafisadi.

Alisema kuwa anashangazwa na agizo la Serikali kushusha bei ya sukari nchini ambayo imepanda mpaka kufikia Sh 2000 kwa kilo moja kutoka katika bei ya kawaida iliyokuwapo ya Sh 1600.

“Watanzania agizo hilo la Serikali limetokana na maandamano ya leo waliposikia tuna andamana kupinga mfumuko wa bei pamoja na Dowans kutokulipwa kwa kodi za wananchi na wao wakajifanya kutoa agizo hilo, ”alisema Mnyika.

Wabunge wa Mwanza
Kwa upande wa wabunge hao wa Chadema mkoani Mwanza waliohudhuria mkutano huo walisema kuwa watahakikisha wanainua maisha ya wana-Mwanza kwa kusimamia rasirimali zilizopo mkoani hapa na kuifanya wilaya ya Bunda ambayo ndiyo ya kwanza kwa umasikini kuondoka kwenye nafasi hiyo .

Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje alisema kuwa ni aibu kwa wana-Mwanza kuchachuka na maisha wakati mkoa huu uonaongoza kwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo kama zitasimamiwa ipasavyo zitawakomboa wananchi wake.

Maandamano ya Mwanza yamefanyika takribani miezi miwili tangu kutokee mauaji ya raia waliopigwa risasi na polisi mkoani Arusha, wakati walipokuwa wakizuia maandamano ya Chadema mkoani humo.

Katika tukio hilo la Januari 6, mwaka huu polisi wa Arusha walimwaga damu za watu kadhaa na wengine zaidi ya 30 walijeruhiwa miongoni mwao wakiwamo walioshiriki na wasioshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chadema.

Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano hayo, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Ispekta Jenerali Said Mwema ambaye awali aliyapiga marufuku baada ya awali kuwa yameruhisiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye.




JIJI la Dar es Salaam lilitaharuki kufuatia milipiko mikubwa ya mabomu iliyotokea ghala la kutunzia silaha la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongolamboto, huku kukiwa na taarifa za watu kufa na zaidi ya 100 kujeruhiwa. Timu ya waandishi wa Mwananchi waliotembelea eneo la tukio usiku wa siku hiyo, walishuhudua nyumba kadhaa zikiteketea kwa moto baada ya kuangukiwa na mabomu.

Kadhalika waandishi hao wa Mwananchi walishuhudia nyumba moja ambayo ukuta wake ulibomoka baada ya kuangukiwa na bomu na ukuta huo kuangukia kundi la zaidi ya watu 12, watu watano wanadaiwa kufa.

Mmoja wa walionusurika kwenye tukio la kuangukiwa na ukuta, Juma Nganyanga, alisema kuna uwezekano ya maiti wengine kuwa chini ya ukuta huo.

Nganyanga alisema aliona kundi la watu wakiwa wamekimbilia kupumzika kwenye baraza la nyumba hiyo baada ya kukimbia nyumba zao, wakati wakiwa katika maombi ya kuomba Mungu awaepueshe na janga hilo, ghafla aliona vumbi likitimka kwenye nyumba hiyo.

Mwenye nyumba hiyo, Farida Magwa, ambaye alikuwa akibubujikwa na machozi alisema akiwa barabarani na familia yake, aliambiwa kuwa nyumba yake imepigwa bomu na kuna watu wameuawa.

Magwa alisema baadaye waliweza kutoa maiti za watu watano, wakiwamo watoto wawili, lakini kuna uwezekano wa wengine bado wapo wamefunikwa na kifusi cha ukuta huo.

Katika tukio jingine, Mwananchi ilishuhudia maiti ya mwanamke ikiwa kwenye nyumba ambayo imeteketea baada ya kupigwa na bomu eneo la Mzambarauni na maiti nyingine ikipandishwa kwenye gari eneo la gereza la Ukonga.

Pia, Mwananchi lilishuhudia jengo la hosteli ya Kanisa Katoliki Ukonga likiwa linateketea kwa moto baada ya kuangukiwa na bomu, huku wakazi wa hosteli hiyo wakiwa wamekimbia.

Moto huo ambao ulikuwa ukiendelea kuwaka hapakuwapo na jitihada zozote za kuweza kuuzima, kwani watu wote walikuwa wamekimbia.

Mlinzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT) lililopo jirani na hosteli hiyo, alisema alishuhudia mabomu mawili yakitua eneo hilo, moja likitua kwenye nyumba ya hosteli hiyo na lingine pembeni karibu na gereza la Ukonga.

Milipuko hiyo ilianza majira ya saa 2.00 usiku na kuendelea mfululizo hadi saa 6.00 usiku, huku watu wakitaharuki na baadhi ya wanandungu na familia kupotezana.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq, alithibitisha kutokea kwa kifo cha mtu huyo ambaye hata hivyo jina lake lilikuwa halijafahamika.

Katika Hospitali ya Amana, Ofisa Mwandamizi wa Wagonjwa wa Nje, Mussa Wambura, alisema watu wawili walifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo na kwamba, hadi saa 7:00 usiku walikuwa wamepokea majeruhi 88, wengine hali zao zikiwa mbaya.

Waandishi wa Mwananchi walishuhudia magodoro yakiwa yametandikwa nje ambako wagonjwa walikuwa wamelazwa na wahudumu wa afya kutoka hospitali za TMJ na Hindu Mandal walipelekwa Amana kuongeza nguvu.

Pia, Sadiq alithibitisha kujeruhiwa kwa watu 43 na kwamba, serikali ya mkoa ilikuwa imetenga hospitali mbili za Ilala (Amana) na Temeke kwa ajili ya kupokea majeruhi na kuwatibu.

Awali, taarifa za zisizo rasmi zilizolifikia Mwananchi zilidai kuwa, mabomu yaliyolipuka ni ya masafa marefu.

Taarifa hizo zilithibitshwa na Sadiq ambaye aliwanukuu JWTZ wakisema, mabomu yaliyolipuka yanaweza kwenda umbali wa kilomita 11 kutoka eneo la tukio, Gongolamboto.

Alisema kwa mujibu wa taarifa hizo, wananchi walipaswa kuondoka eneo hilo na kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam na kwamba, wangekuwa salama baada ya kufika eneo la Tazara wakati kwa wale walioelekea Kisarawe alipaswa kwenda hadi eneo la Pugu Kajiungeni.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi, Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, alinukuliwa akiwataka wakazi wa Gongolamboto na maeneo ya jirani kuhama makazi yao kutokana na milipuko hiyo.

Kadhalika Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alinukuliwa akiwataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kuepusha athari zinazotokana na milipuko hiyo.

Wananchi wakimbia makazi
Habari zaidi zilisema mamia ya wananchi waliyakimbia makazi yao, wengi wakielekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam, lakini baadaye matangazo yaliyotolewa na vyombo vya usalama yaliwataka kwenda Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kupata hifadhi ya muda.

Kwa mujibu wa mashuhuda, watu walikuwa wakikimbia ovyo huku wakipanda magari yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji, kusalimisha maisha yao.

Baadhi ya wananchi waliolazimika kuyakimbia makazi yao, walikuwa wakipiga simu chumba cha habari wakilalamikia kupotezana na ndugu zao.

Mamia ya watu kutoka Gongolamboto, Karakata, Tabata, Segerea, Ukonga, Kitunda, Banana na maeneo mengine jirani, walionekana wakipanda daladala, wengine wakining'inia nyuma ya magari hayo yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji, huku mamia kwa mamia ya watu walikuwa wakitembea kwa miguu kuokoa maisha yao.

Kadhalika pikipiki, bajaj na magari ya kama pick-up pia yalitumika kuwahamisha watu kutoka eneo la tukio kwenda kutafuta sehemu ya hifadhi ya muda.

Uwanja wa ndege wafungwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, ulifungwa kwa muda na ndege zote hazikuruhusiwi kuruka wala kutua hadi hapo itakapoarifiwa baadaye.

Waandishi wa Mwananchi walishuhudia abiria wengi wa kigeni wakiwa kwenye uwanja wa huo wakisubiri kujua hatma ya safari zao, baada ya ndege walizokuwa wakizisubiri kuamriwa kutua viwanja vya Kia na Zanzibar hadi hapo watakapopewa maelekezo mengine.

Barabara ya Pugu katika njiapanda inayoingia kambi ya jeshi, ilifungwa na magari yote yaliyokuwa yakielekea katikati ya jiji na yale yaliyokuwa yakielekea Kisarawe yalizuiwa.

Mkazi mmoja wa Kigamboni aliyepiga simu ofisi za gazeti hili jana usiku wakati milipuko ya mabomu hayo ikiendelea, alisema wakazi wengi wa Kigamboni walikuwa nje ya nyumba zao, huku wakishuhudia makombora yaliruka juu kuelekea baharini hali ambayo iliwafanya wakazi hao kukumbwa na wasiwasi mkubwa.

"Hivi ninapokupigia wewe, makombora yanapita juu na kila mtu na familia yake wako nje kwa hofu...unasikia muungurumo huu kombora jingine linapita hapa juu kuelekea baharini," alisikika mwananchi huyo.

Kauli ya Dk Mwinyi
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Mwinyi, alisema milipuko hiyo ilitokea ghala namba tano na kwamba, kilichokuwa kikifanyika ni kuzuia usienee sehemu nyingine.

Dk Mwinyi alisema kambi ya Gongo la Mboto wanaishi wanajeshi na familia zao, lakini maghala ya mabomu yako mbali na kuongeza kuwa, kutokana na milipuko hiyo kuwa mikubwa hawezi kuzungumzia athari.

“Ile ni kambi ya jeshi, watu wanakaa mbali na maghala lakini kwa sababu tukio lenyewe ni kubwa sasa hivi hatuwezi kusema lolote,” alisema Dk Mwinyi.
Wakati mabomu hayo yakiendelea kulipuka mwananchi mmoja alipiga simu chumba cha habari cha Mwannchi, akisema Waziri Mwinyi yalipolipuka mabomu ya Mbagala, aliahidi kujiuzulu iwapo ingebainika kulifanyika uzembe.

Hata hivyo, Dk Mwinyi alipoulizwa usiku wa kuamkia leo kuhusu utekelezaji wa ahadi yake hiyo na majibu ya tume zinazoundwa, alisema kilichokuwa kinafanyika usiku ni kuokoa maisha ya watu, masuala mengine yatazungumzwa baadaye.

“Sasa hivi kuna jambo linaathiri watu, kwanza tuwaokoe halafu haya mengine tutazungumza,” alisema Dk Mwinyi.
Milipuko ya kwanza ilitokea barabarani mwaka 1972 wakati mabomu hayo yalipokuwa yanahamishwa kutoka Kambi ya Kunduchi kwenda Gongolamboto.

Kwenye kambi hiyo ni mara ya pili kutokea kwa milipuko ya mabomu, milipuko ya kwanza ilitokea mwaka 2008 na kusababisha maafa kwa wananchi wanaozunguka kambi hiyo, wanajeshi na familia zao.

Thursday, February 24, 2011

MBONA WANANGANGANIA HAPO KATI?



Mh jamani mbona wanangangania hapo kati kunanini hata wewe dd.

Thursday, February 10, 2011

DOGO DITTO


Dogo ditto mkari wa THT AKITUMBUIZA WAKTI WA SHEREHE ZA MIAKA MI 5 YA tht ndani ya ukumbi wa MLIMANI CITY.

Tuesday, February 8, 2011

SHILOLE THE NEW ACTRESS IN BONGO



Huyu ni shilole ni msanii mpya wa kike kwenye firam za kibongo kwa sasa.

Saturday, February 5, 2011

ALI CHOCKY NA WANAMUZI WAPYA


KIONGOZI WA BENDI YA EXTRA BONGO ALLY CHOCKY AKIWA NA WANAMUZI SITA WALIOTOKA TWANGA PEPETA.

THIS IS KIM K



hapo vp jamani.

THIS IS MBONI MASIMBA ALSO



PLEASE ADVISE ME TO BELIEVE FOR THEIR SHAPE LOOK LIKE.

IS IT MBONI LOOK LIKE KIM K?


Tuesday, February 1, 2011

Giggs: United's greatest


After six weeks of voting and thousands of submissions, United fans have crowned Ryan Giggs the club’s greatest ever player, topping a poll held by the club’s official magazine, Inside United, and ManUtd.com.

Welsh winger Giggs was typically magnanimous when he found out he’d won. “When I got told I was really chuffed,” he said.

“I couldn’t believe it to be honest, especially when you look at the list of other players who are up there.”

The Greatest: The Top 10
As voted for by readers of Inside United and ManUtd.com, the Reds' top 10 players of all time are as follows:

1. Ryan Giggs
2. Eric Cantona
3. George Best
4. Sir Bobby Charlton
5. Cristiano Ronaldo
6. Paul Scholes
7. David Beckham
8. Roy Keane
9. Peter Schmeichel
10. Wayne Rooney